kiswahili mufuti Gredi 1

0
(0)
0 10732
USh 25,000
In Stock
G202K23132C0
God's Mercy Bookshop

Longhorn Kiswahili Mufti, Gredi 1 (Kitabu cha Mwanafunzi) ni kitabu kilichoandikwa kwa mtindo wa mazoezi kwa kuzingatia mtaala mpya unaokusudiwa kujenga ujuzi wa mwanafunzi kupitia utendaji na uvumbuzi wa maarifa. Kitabu hiki kimetimiza kikamilifu mahitaji ya mada zote za silabasi mpya ya somo la Kiswahili kwa wanafunzi wa gredi ya kwanza.

Vilevile, kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha rahisi ili kueleweka kwa urahisi na wanafunzi wa gredi ya kwanza kutoka katika mazingira mbalimbali. Msamiati uliotumika unaafikiana vyema na uwezo wa lugha ya wanafunzi katika kiwango hiki. Kimeshughulikia masuala ibuka kama vile: maadili, haki za watoto, usafi na afya, utangamano, maarifa ya ujasiriamali, elimu ya maendeleo endelevu, jinsia, teknolojia na mazingira.

Pia, michoro ya kuvutia imetumiwa ili kumsaidia mwanafunzi kufahamu yaliyomo kwa urahisi na kuweza kuyahusisha maarifa na mazingira yake.

Kitabu hiki kina mwongozo wa mwalimu ambao utampa mwalimu maelezo na maelekezo kamili kuhusiana na mbinu mwafaka za kutayarisha, kuendesha na kutathmini uwezo wa utendaji wa wanafunzi na umahiri wao katika somo la Kiswahili.

Shipping Cost
Shop Location God's Mercy Bookshop, Namirembe Road, New taxipark building, Unit 674, Central Region, Uganda

No reviews found.

No comments found for this product. Be the first to comment!