Kitabu cha Kiswahili cha Baroque cha wanafunzi wa kidato cha kwanza kimeandikwa kulingana na mtaala mpya wa vidato vya msingi vya shule za upili, wenye lengo la kuwezesha wanafunzi kuwa na uamuzi wa busara kama wananchi na wanafamilia na pia kuwapatia uwezo wa kupata mafunzo yanayowawezesha kufikiria kihakiki na kujifunza vizuri.
Kitabu cha wanafunzi kimetungwa kwa msisitizo wa kujenga stadi kuu nne za ujifunzaji kusema, kusikiliza, kusoma na kuandika. Katika mafunzo yao kwa Kiswahili, wanafunzi wataongezea kwa stadi zao walizozimudu katika kiwango cha shule za msingi kwa kufahamu na kushiriki kiundani, katika mawasiliano tofauti na mazungumzo yenye ufasaha. Katika ujifunzaji, wanafunzi pia watajenga stadi za kibinafsi na za uhusiano na wengine pamoja na kujenga umoja, ambapo ni muhimu sana katika maisha na katika dunia ya utendaji.
Kitabu hiki hujumlisha mitindo tofauti ya ufundishaji na ujifunaji pamoja na mahitaji, ambayo yatawezesha wanafunzi kujenga stadi zitakazowasaidia kujieleza kiubunifu na kufikiria na kuwasiliana vizuri na wengine.
Vipengele muhimu vifuatavyo vimezingatiwa katika uandishi wa yaliyomo kitabuni; heshima kwa maisha ya binadamu, kufahamu umuhimu wa kuishi kwa maelewano katika mazingira, uhuru na kufikiria kihakiki. Kutenda, kuweza kubadilika pamoja na
kubadilisha jamii.
Kwa kufikia mwisho wa mafunzo haya, mwanafunzi aweze:
• Kuwajibikia ujifunzaji;
• Kujifikiria na kuwa ufahamu wa dhana tofauti;
• Kuwa mfikiri wa kihakiki ambaye yuko tayari kupambana na hali na changamoto
mpya;
• Kuwasiliana vizuri na wengine.
ISBN | 9789970470228 |
Стоимость доставки |
|
Перевозки | 1-2 дня |
Product Location | GODS MERCY BOOKSHOP, New taxipark, Freeman building, Shop 674, Central Region, Uganda |
Отзывов не найдено!
Нет комментариев к этому продукту. Прокомментируйте первым!